WATANZANIA

Watanzania Wazalendo Watalii wa ndani pamoja na Ndugu wapendwa  wasomaji  na Watazamaji wetu  wa Tovuti hii inatupasa sisi sote tunapokuwepo hifadhini katika matembezi ya uangaliaji  wa viumbe hai wanyamapori pamoja na uoto wake  wa asili popote pale nchiniTanzania tukafahamu ya kwamba kila mmoja wetu miongoni  mwetu  anawajibika kujifunza na kuchanganua  mazingira  ya  makazi  ya viumbe  wanyamapori  wanayoishi  na kupatikana katika  sehemu  zake  husika za kimakazi na vile vile  kila  mmoja  wetu  miongoni  mwetu  anatakiwa  akawafahamu  kwa njia moja  ama  nyingine katika kuwaelezea  viumbe  hai  wanyamapori  kwa Watanzania  wenzake  na jamii kwa ujumla  katika sehemu  anayopatikana  kwa njia ya kujifunza  na kujielimisha kutoka  kwa wengine  katika kuleta   hamasa  kwa  wengineo  ambao  hawajawahi  kabisa  kutembelea  hifadhini.  Kwa njia hii  itasaidia   kuwaelezea  Wanyamapori  mmoja mmoja pamoja na  majina  ya  Kisayansi  na yale  ya kawaida  ili kupata  kuwa na mtiririko  wa kitaalamu  wa viumbe  hai wanyamapori  na  mimea  katika safari ya  matembezi  ya  Kitalii  hifadhini. 

     Ikumbukwe  na ieleweke  ya kwamba  hatua  nyingineyo  inayofuata  baada ya hapo  ni  katika utambuaji wake  mnyamapori  husika pamoja  na mazingira  ya makazi yake  anayo yapendelea   kuishi,  chakula anachokula,  maadui zao  husika na vile vile  wakati  mwingine  njia  za uhamaji  wake kimsimu. 

     Hatua ya mwisho kabisa ni taboa ya mnyamapori pamoja na asili yake  kihistoria.  Kumfahamu  mnyamapori  tabia yake  kwa undani  na  mapana  yake  basi  hii  inaonyesha  ya kwamba  unafahamu ipasavyo  umuhimu  wake  mnyamapori husika.  Kipindi cha wakati  ulio bora  na maeneo  kwa utazamaji   viumbe   hai  wanyamapori  ni  pasipokuwabugudhi wanyamapori.  Mwisho  kabisa  ikumbukwe  na ieleweke  kwa wasomaji  na watazamaji  wetu  pamoja na  watanzania  watalii wa ndani   kwa ujumla  wake  ya kwamba  wanyamapori  wakati  wote  ni rahisi  kuwaona  kwa kipindi  cha  muda  ulio  mrefu  hususani  katika  mazingira  ya makazi  ya uoto wa nyasi  (Grassland)  na  vile vile   maeneo  ya mapori  yasiyofunga  ambapo  binadamu   ndio  asili  yetu  tulikotokea.

Edgardo Kabulwa Welelo, Moshi, Kilimanjaro, Tanzania. | Barua pepe:  edgardowelelo@yahoo.com

TAZAMA NA SOMA SEHEMU YA KIPENGELE CHA  “ELIMIKA” ILI  UWEZE KUPATA KUJIFUNZA NA KUJIELIMISHA IJAPOKUWA KWA KIASI KIDOGO  YALE YOTE YALIYOKWISHA KUELEZWA KATIKA SEHEMU  HII.

Tanzania.
Tanzania inakadiriwa kuwa na jumla ya viumbe hai zaidi ya milioni 4.  Miongoni mwa viumbe hai wanyamapori  wanaopatikana  na kuonekana  popote  pale  nchini  Tanzania  pasipokuwepo  shida  yeyote  ile  ni  pamoja  na pundamilia, Tembo au ndovu,  nyumbu, mbogo au nyati, viboko, pofu, Twiga, Tandala wakubwa  na wadogo,  Korongo, Pongo, Swala tomi,  Swala granti,  Nyamera pamoja  aina  mbalimbali  ya wanyamapori  aina ya  swala.  Vile vile  kuna   viumbe  hai   wanyamapori  walaji  wa nyama  kama vile   fisi,  mbwa  mwitu,  samba  pamoja na chui  na vile vile  hali  kadhalika  pasipokusahau viumbe  hai  wanyamapori   jamii  ya nyani  (Primates)  kama  vile  sokwe  mtu  katika  maeneo  ya hifadhi  za Taifa  Mahale  pamoja  na Gombe  Mkoani  Kigoma.  Tanzania  vile vile  ina zaidi  ya  viumbe  hai  wadudu  60,000 na takribani  aina  25  tofauti  ya viumbe  hai  reptilian  na hii inahusisha  takribani  aina  100  mbalimbali  za nyoka,  amphibian  pamoja na Samaki.

Tanzania  vile vile  ni  sehemu  pekee duniani  kwa  kuwa  na utajiri  wa  mali asili  viumbe  hai ndege  na inakadiriwa  kuwa  na zaidi ya  viumbe  hai  ndege  1000 mbalimbali  na  hii ni  pamoja ndege  wa makazi  ya  maji,  misitu,  savanna na baharini.  Kwa wapenzi  watazamaji  wa viumbe  hai ndege  watarajie  kuona  viumbe  hai ndege  kama vile  Mbuni, Kanga,  Tandawala, kwale  Udzungwa,  Korongo,  kichwa  nyundo,  Heroe,  Hondo hondo na wengineo  walio wengi.

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
free hit counter

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU