UTAMBULISHO

Dondoo: Tazama Ramani Tanzania ni Tovuti huru ya kielimu, Kizalendo, kitaifa na kijamii nchini Tanzania ambayo si ya kiserikali inayoendeshwa, kuratibiwa na kisimamiwa na chuo cha Utalii cha Udzungwa kinachopatikana Mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro (www.udzungwamountainscollege.com). kilichojikita mizizi yake zaidi katika uelimishaji na uhamasishaji utalii wa ndani na mazingira yake kwa watanzania wazalendo watalii wa ndani.

Uanzishwaji wa tovuti hii umetokana na tathmini ya chuo chenyewe katika eneo hili la utalii wa ndani na uzoefu wake kivitendo katika uhamasishaji na uelimishaji wa utalii wa ndani kwa umma wa watanzania tangu mwaka 2008 na vile vile maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Taifa letu Tanzania tarehe 9/12/2011. Hizi ni jitihada zetu binafsi kama moja ya taasisi za Kielimu katika kuiunga mkono Serikali yetu na Wizara yake mama ya maliasili na utalii, Bodi ya utalii, Shirika la hifadhi za Taifa na mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro na wadau wengineo katika sekta ya utalii katika kuongeza idadi ya Watanzania watalii wa ndani kutembelea vivutio vyetu asilia vya utalii nchini Tanzania. Tukiamini ya kwamba kila mtanzania mzalendo wa nchi hii anawajibika katika kutangaza utalii wa nchi yetu kwa wananchi wenzake na wageni watalii kutoka nje ya nchi yetu kwa nafasi yake aliyonayo popote pale. Mpango mkakati wa Tazama ramani Tanzania ni kuwawezesha na kuwafanikisha watanzania zaidi ya milioni ishirini (20) kutembelea vivutio vyetu asilia vya utalii Tanzania kwa vitendo ifikapo mnamo mwaka 2020 kwa kuwaelimisha na kuwahamasisha watanzania wote wa umri wowote ule na wa tabaka zote kwa njia mbalimbali kama vile Jarida lake la Tazama ramani Tanzania, maonyesho ya utalii, makala katika televisheni, vitabu vya viongozi (Guide books), mipango maalumu katika shule na vyuo,ramani,kanda za video pamoja na Dvds.

Safari za matembezi ya utalii wa ndani yanayoratibiwa, kusimamiwa na kuendeshwa na Chuo cha Utalii cha Udzungwa cha Mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro (www.udzungwamountainscollege.com) zilianzishwa tangu mwaka 2008 na kupelekea kuwepo kwa uanzishwaji wa Kampuni ya utalii wa ndani katika uelimishaji na uhamasishaji utalii wa ndani (www.domestictourismsafaris.com) na hatimaye hivi sasa Tovuti ya Kiswahili, Jarida la Tazama ramani Tanzania na vitabu vya viongozi vya kiswahili.

Katika kutoa fursa kwa Watanzania watalii wa ndani, safari zetu za matembezi hifadhini katika maeneo tofauti ya hifadhi za Taifa na maeneo mengineyo ndio yakamilishayo dhamira yetu ya kuwaelimisha na kuwahamasisha watanzania wote wa umri wowote ule na wa tabaka zote kuwa wapende mazingira na kutangaza vivutio vyetu asilia vya utalii nchini.

DHAMIRA YA MTANDAO Kufikia Mamilioni ya watanzania watalii wa ndani kupitia jarida lake la utalii wa ndani la Tazama ramani Tanzania, vipindi maalumu katika redio na Televisheni, makala katika televisheni, vitabu vya viongozi vya utalii (Guide books), kanda za video na Dvds, Ramani na vyombo vya habari mbalimbali nchini Tanzania. - See more at:

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
free hit counter

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU