MAZINGIRA

UOTOSHAJI JOTO DUNIA (GLOBAL WARMING) IMEKUWA HALI HALISIA YA UKWELI WA MAMBO – HILI NI JANGA LA KITAIFA NA DUNIANI

Ni ukweli  halisi wa mambo ulio wazi duniani  popote  pale  ya kwamba  mabadiliko  ya tabia  ya nchi  yanashika   kasi sana  kwa sababu  ya uotoshaji joto Duniani (Global warming). Sote kwa pamoja popote pale duniani tunakabiliana na tatizo la mabadiliko ya Tabia ya nchi (climate crisis).

          Kama hatutaweza  kulitambua  hili basi  ieleweke  ya  kwamba  ni  tatizo  halisia  na   inabidi sote  kwa pamoja   tuweze   kushirikiana  na kushikamana katika kuchukua  hatua  thabiti  katika  utekelezaji  kwa njia ya vitendo. Sisi  binadamu  duniani kote  ndio  chanzo  kikubwa  kisababishacho tatizo  hili la  uotoshaji  joto  duniani.  Na ni wajibu wa kila Mtanzania kuwajibika katika kupambana na tatizo hili.

MLIMA KILIMANJARO PAMOJA NA KUTOWEKA KWA ZIWA MANYARA
Mlima Kilimanajro katika nchi yetu  Tanzania na  Afrika hapo zamani  ulikuwa  umefanikiwa  theluji  karibia  maeneo  yote  ya vilele vya Mlima  Kilimanjaro. Theluji ya mlima Kilimanjaro pamoja  na maeneo  mengineyo duniani popote  pale inazidi kutoweka  katika  kasi  ya kutisha  sana.

          Karibia  theluji  zote  katika vilele  vya  milima  duniani  inaendelea  kuyeyuka  katika kasi ya kupindukia  sana.  Theluji za milima  ya Tibeti ni miongoni mwa maeneo yaliyoathirika na uotoshaji joto dunia (Global warming). Wanasaynasi duniani wanaeleza ya  kwamba  theluji  hizi  katika milima  ikitoweka  katika kipindi  cha ndani  ya Nusu  karne ijayo, takribani idadi ya  watu duniani bilioni 2  nukta 6 itakaribiwa  na tatizo  sugu la upatikanaji  wa maji  duniani  mpaka  pale  tu ambapo  jamii ya  kimataifa  itakapowajibika  ipasavyo katika  kukabiliana  na tatizo  hili  kwa  haraka  iwezekanavyo na vile  vile  katika  utekelezaji wake  kwa njia  ya vitendo. 

 KUTOWEKA  KWA  ZIWA   CHAD.
Katika  Afrika  ya kati  kulikuwepo  ziwa  kubwa   sana  lionalofahamika  leo hii kama ziwa  CHAD.

          Takribani miaka 40 ziwa Chad lilikuwa  moja  ya maziwa  sita makubwa  duniani. Jamii  za watu  zilizokuwa  zikiishi  jirani  na ziwa  Chad  kama vile  nchi za  Chad, Nigeria, Cameroon na  Niger  zilitegemea  sana  chanzo cha maji  ya ziwa  CHAD  kwa  ajili ya  kilimo  cha  umwagiliaji, Uvuvi, mifugo na  matumizi ya nyumbani.  Kwa sababu  ya  kuwepo  upungufu  wa  upatikanaji  wa Mvua na kuongezeka  kwa mahitaji  ya  matumizi ya Ziwa CHAD, lilipelekea  kupungua sana  ukubwa  wa eneo  lake. 

KUONGEZEKA KWA IDADI YA WATU DUNIANI
Ifikapo mwaka 2050 kutakuwepo zaidi ya watu billion 9 duniani kote.  Karibia  duniani  kote   miji  mikubwa  imefurika  kwa  kuwa na watu  wakazi  wengi.  Kwa mfano Jiji la  Tokyo nchini  Japan linakadiriwa kwa  kuwa na idadi  ya watu zaidi ya million 35. Kwa sababu  ya kuongezeka  kwa  kasi ya  idadi  ya  watu  duniani hii  itasababisha  kuwepo  kwa  mahitaji  makubwa  ya  chakula,  makazi, maji na  nishati  ambapo hii zitaathiri upatikanaji  wa mali  asili. Kwa kuwa  idadi  kubwa  ya wakazi  kuishi mijini hii  itasababisha   maeneo  makubwa  ya  misitu  kukatwa  na kutoweka  kwa ajili ya mbao  na chakula  kwa  wakazi  waishio  mijini.

soma zaidi

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
free hit counter

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU