ELIMIKA

Mashirika ya umma ya Hifadhi  za Taifa
(Tanzania National Parks  Authority – TANAPA) na Mamlaka  ya hifadhi  ya Ngorongoro (Ngorongoro conservation Area  Authority – NCAA)  ndio  Mashirika Makuu pekee nchini  Tanzania  yaliyopewa  majukumu, dhamana, pamoja na mamlaka  ya  udhibiti na usimamizi wa kuyalinda na kuyahifadhi  maeneo  ya  uhifadhi yenye kuwa na   mandhari  nzuri  ya   kupendeza  na maumbile  yake  asilia ya Kijiografia  yaliyo  maliasili ya  nchi na  urithi  wetu  kwa maslahi  ya nchi,  Watanzania wote,  vizazi  vyake  vilivyopo  na  vizazi  vijavyo  katika kuvifurahia  na kufaidika navyo. 

HISTORIA YAKE: 
Kwa Watanzania  watalii wa ndani  ni lazima  wakafahamu ya kwamba  Mashirika  haya   yote  kwa pamoja  ya  hifadhi  za Taifa  (Tanzania  National  Parks  Authority – TANAPA) na  Mamlaka  ya hifadhi  ya Ngorongoro (Ngorongoro  Conservation  Area  Authority – NCAA) yalianzishwa  mwaka 1959.

MAJUKUMU YA KAZI  ZA SHIRIKA  LA HIFADHI  ZA TAIFA
Ikumbukwe  na ieleweke  kwa Watanzania watalii wa ndani  ya kwamba  Shirika  la umma  la  hifadhi za Taifa  (Tanzania National  Parks Authority) ndio Shirika  pekee  nchini  Tanzania lenye  kubeba  majukumu ya mamlaka  ya udhibiti na usimamiaji  pamoja na uendeshaji wa hifadhi  zote za  Taifa nchini Tanzania  ambazo  ni  takribani  16 mpaka  hivi sasa.

KAZI ZA SHIRIKA LA UMMA LA HIFADHI ZA TAIFA:
Kuyalinda  na kuyahifadhi  makazi  ya maeneo  ya uhifadhi  yenye  kuwa na maumbile  asilia  ya Kijiografia, mandhari  zake  nzuri  zenye  kupendeza,  viumbe hai  wanyamapori na uoto  wa asili  kuwa mali asili  endelevu  kwa ajili  ya  maslahi  ya nchi  na urithi  wetu  kwa  watanzania  wote, vizazi  vyake  vilivyopo  na  vizazi  vijavyo.
Kupata  pato la fedha za kigeni  linalotokana na mali asili  ya maeneo  ya  uhifadhi  kupitia  utalii wa Kimataifa  katika  kuyaendeleza  maeneo  ya uhifadhi  kuwa endelevu. 

IDADI YA JUMLA YA HIFADHI ZA TAIFA NCHINI TANZANIA; 
Ikumbukwe  na ieleweke  kwa watanzania  watalii wa ndani  ya  kwamba  mpaka  hivi  sasa  hifadhi  za Taifa  ni takribani  16. 

-Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
-Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
-Hifadhi ya Taifa ya Katavi
-Hifadhi ya Taifa ya Mikumi
-Hifadhi ya Taifa ya milima ya Udzungwa
-Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale 
-Hifadhi ya  Taifa ya Milima ya Kitulo
-Hifadhi ya Taifa ya Gombe 
-Hifadhi ya Taifa ya Arusha
-Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara
-Hifadhi ya Taifa ya Tarangire
-Hifadhi ya Taifa ya Mlima  Kilimanjaro 
-Hifadhi ya Taifa  ya Mkomazi 
-Hifadhi ya Taifa ya visiwa  vya Rubondo
-Hifadhi ya Taifa ya Saadani
-Hifadhi ya Taifa ya saa Nane

soma zaidi

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
walio tembelea

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU