Hifadhi ya Taifa ya Katavi

Ukweli kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa.
Hifadhi ya Taifa ya Milima  ya Udzungwa  inapatikana Kijiografia  maeneno  ya  KUSINI  katikati ya  Tanzania yenye kuwa na  ukubwa wa eneo  la kilomita za mraba  1990 na ni eneo  ambalo  asilimia  80 ya ukubwa  wa eneo  lake   linaangukia  Mkoa wa Iringa  katika  Wilaya  ya Iringa Vijijini (Msitu wa asili wa Kilombero Magharibi) na asilimia  20  inapatikana katika  Mkoa wa Morogoro (Wilaya  ya Kilombero, msitu wa asili  wa Mwanihana). 

  Jina Udzungwa asili yake limetokana na Kabila la Wahehe likimaanisha  watu waishio ngambo  ya pili  ya mlima. Hifadhi  hii ya Taifa  ya milima  ya Udzungwa  inaundwa  na maeneo  matano (5)  ya mapori ya akiba  ya  misitu ambayo  ni mwanihana, Kilombero  Magharibi,  Nangaje,  matundu  na Iwonde. Hii  ndio  hifadhi  pekee  nchini Tanzania  ambayo  inapatikana  katika  milima  ya  Tao la Mashariki  (Eastern  arc) na vile vile  ndio  hifadhi  ambayo  ina  wanyamapori jamii  ya nyani  (primates)  zaidi ya  Tisa  (9).  Vile  vile  ni hifadhi  pekee  nchini  Tanzania  ambapo umeme  unaozalishwa  kwa njia ya maji  takribani  asilimia 70  hutokea  katika  hifadhi  hii.

MAANDALIZI YA USAFIRI:
Tafuta  na kusanya  taarifa  zote  zinazohusiana na wadau wa Sekta ya utalii  watoao huduma za utalii  katika hifadhi  ya Milima  ya Udzungwa. Taarifa hizo  zipatikanazo ndizo zitakazowezesha  kuandaa  mpango  mkakati  wa kutembelea  hifadhini. Haya ndio mambo muhimu ambayo yatakayotoa hali halisi ya fedha  zitakazohitajika na jinsi zitakavyotumika.

KUANZISHWA KWAKE:
Ilianzishwa  mnamo  mwaka wa 1992.

ENEO LAKE:
Hifadhi  hii ya Taifa ya  Milima ya Udzungwa ina ukubwa   wa eneo  lenye  kilomita za mraba  1990.

UFIKAJI HIFADHINI:
Hifadhi  ya Taifa  ya milima  ya Udzungwa  inafikika  umbali  wa kilomita  350 kwa  njia ya  barabara,  Kusini  magharibi   kutoka Mkoani  Dar es salaam,  takribani  saa 6. Vile vile kilomita 75 kutoka mji wa Mikumi na hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

  Makampuni kadhaa ya usafiri wa mabasi yanatoa huduma za usafiri kupitia hifadhini kutoka Dar es salaam na Ifakara.  Wasiliana  na wakala wa usafiri kwa maelezo zaidi. Vile vile kuna  lango  la  kuingilia  upande  wa  Magharibi. Lango la Msosa ni kilomita 10 kutoka Mtandika. Na lango  la  udekwa  ni  kilomita  63  kutoka  Ilula katika  barabara kuu  ya Dar – es – salaam -Iringa.

MAUMBILE ASILIA YA KIJIOGRAFIA HIFADHINI:
Aina mbali mbali  za sura ya eneo  kama  vile  vilima,  milima,  mabonde,  maporomoko ya maji,  mandhari  ya eneo  zuri  yenye  kupendeza. Vile vile  kuna  vilele vya  milima,   uoto wa asili  wa msitu wa Mlimani, wanyamapori jamii ya  nyani  (primates)  kama vile mbega  wenye  rangi  nyeusi  na nyeupe na mbega  wekundu,   kima na wengineo wengi.  Viumbe  hai  ndege   ni pamoja  na kwale  Udzungwa  ambao  hupatikana pekee  hifadhini  Udzungwa.

soma zaidi

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
free hit counter

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU