Hifadhi ya Taifa ya Katavi

Ukweli kuhusu hifadhi ya Kitulo,
Hifadhi ya Taifa  ya milima  ya Kitulo  inapatikana  kijiografia  katika  nyanda za juu  Kusini  Mkoani  Mbeya  takribani  kilomita  100  kutoka  jiji la  Mbeya.  Ni  hifadhi  ambayo  imetawaliwa  na uoto wa asili  wa  Maua  na  wakazi  Watanzania  wenyeji wa maeneo haya  wameipa  jina la bustani  ya Mungu.

MAANDALIZI YA USAFIRI:
Iwe usafiri binafsi au usafiri wa kukodi ni lazima fungu la fedha litengwe pembeni   ili kufanikisha safari ya matembezi hifadhini Kitulo. Vitu  gani  ambavyo  ni muhimu vinavyohitajika na vitu  gani  visivyohitajika  ni suala  la utafiti  wa kuangalia  na kupata  maelezo  ya kina  kuhusiana na  sehemu  hii mnayokusudia  kuitembelea. Taarifa na maelezo ni mambo muhimu na yanayohitaji kupewa kipaumbele cha hali ya  juu  kabisa.

KUANZISHWA KWAKE:
Ilianzishwa rasmi mwaka 2005.

ENEO LAKE:
Ukubwa wa eneo la hifadhi ya milima ya Kitulo ni kilomita za mraba 412.  Na  uwepo wake  kijiografia katika nyanda za juu  Kusini  kunapelekea  hifadhi  hii hali yake  ya hewa kuwa ya baridi  na mwezi  wa Juni  na Agosti inakuwa  ni baridi  sana. Mvua ni nyingi na joto kawaida ni la chini. 

UFIKAJI HIFADHINI:
Kwa njia ya  usafiri  wa barabara, hifadhi hii inafikika kutoka  Chimala,  takribani  kilomita  78 Mashariki  ya Jiji la  Mbeya  katika  barabara kuu  iendayo Dar es – salaam,  katika uelekeo wa Kusini  katika  barabara  ya  vumbi  ijulikanayo “ Hamsini na saba”.

          Ni takribani  saa mbili kufika  katika makao  makuu ya muda  mfupi  ya hifadhi  hii iliyopo  Matamba   ambapo  inachukua  mwendo  mfupi  tena  kufika hifadhini. 

MAUMBILE ASILIA YA KIJIOGRAFIA HIFADHINI:
Uoto wa asili,  Mandhari  nzuri  ya kupendeza  ya milima,  uoto wa asili  wa milimani.

HALI YA HEWA USAWA WA BAHARI HIFADHINI:
Mita 2600 baina ya vilele vya milima kipengere, mporoto na Livingstone. 

VIVUTIO VIKUU VYA UTALII HIFADHINI:
Maua ya porini, mimea mikuu, aina kadhaa za viumbe hai ndege, vipepeo, vinyonga, mijusi pamoja na vyura.

soma zaidi

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
free hit counter

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU