Hifadhi ya Taifa ya Katavi

Ukweli kuhusu hifadhi ya Mlima Kilimanjaro:
Ukweli halisi  wa mambo  jina “Kilimanjaro” kutokana na maelezo ya wenyeji asilia  wachaga wa Mkoa huu waishio maeneo haya ya mlima ni kwamba neno “Kilimanjaro”limetokana na neno   la Kabila  la Wachaga “Kilema Kyaro” likimaanisha  safari  iliyoshindikana au isiyowezekana . “Kilema’ inamaanisha  kisichowezekana  au  kilichoshindikana na neno “Kyaro” likimaanisha safari. Tafsiri rahisi hapa  ina  maana ya  kwamba  safari  ya matembezi kuelekea kupanda kilele cha mlima kilikuwa  kikiwashinda watu wengi waliojaribu  kupanda mlima na hii ilikuwa  wakati wa kipindi  cha nyakati  hizo za miaka ya zamani.  Leo hii hali  hiyo  haipo tena kwa sababu  wengi  wa watalii  kutoka  nje ya  nchi  na ndani  ya nchi  hufika  kileleni  mwa  mlima  pasipo shida yeyote  ile. Hifadhi  hii kama inavyojieleza,  kijiografia  inapatikana mkoani  Kilimanjaro.

kileleni

MAANDALIZI YA USAFIRI:
Utalii ni burudani na vilele  ni sehemu ya mafunzo ya kielimu. Hivyo  basi,  kwa njia  yeyote  ile iwe au isiwe,  fedha zinahitajika  katika  maandalizi ya kupanda mlima. Ufanisi wa kufanikisha  maandalizi ya matembezi  ya mguu katika  kupanda  mlima utategemea  zaidi jinsi  fedha zitakavyotumika na  mpangilio wa bajeti  ya fedha  hizo.

KUANZISHWA KWAKE.
Hifadhi  ya mlima  Kilimanjaro ilianzishwa  rasmi  mnamo  mwaka 1973.

UFIKAJI  HIFADHINI:
Hifadhi  ya Taifa ya mlima  Kilimanjaro inafikika kwa njia ya barabara  umbali  wa kilomita 48 kutoka  mji  wa Moshi  ambao  ndio  makao  makuu ya mkoa  wa Kilimanjaro. Vile vile hifadhi hii  inafikika umbali wa kilomita 128 kutoka  mkoani  Arusha. Inachukua  mwendo  wa dakika  50 kutoka  Moshi  Mjini, vile vile  ni  mwendo  wa saa 1 kutoka  kiwanja  cha ndege  cha  kimataifa cha  Kilimanjaro (KIA). Hali kadhalika ni saa 2.30 kutoka  mkoani  Arusha. 

soma zaidi

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
free hit counter

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU