Hifadhi ya Taifa ya Katavi

Ukweli kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Katavi:
Hifadhi ya Taifa  ya Katavi  inapatikana  katika  Wilaya  ya  Mpanda,  Mkoani Katavi,  ambao ni Mkoa mpya uliogawanyishwa  kutoka Mkoa wa Rukwa  kama jinsi  ilivyokuwa  ikijulikana  hapo zamani . Jina la hifadhi  hii ya  Katavi  inatokana na jina asili  la mwindaji  maarufu  wa Kienyeji aliyeishi  maeneo  haya  ya  hifadhi  aliyejulikana  kama “KATABI”.

viboko

          Hifadhi hii inapatikana  kimipaka na  maeneo ya mapori ya akiba ya wanyamapori ya Rukwa  kwa  upande  wa Mashariki, Kaskazini mwa barabara  ya Sitale  Inyonga na Magharibi  ya mto  “KAVUU”.

MAANDALIZI YA USAFIRI:
Fedha  itafutwe  na iandaliwe  kwa  umakini  mkubwa  kimatumizi na kiuhitaji katika  safari  yenu  ya matembezi  hifadhini.

KUANZISHWA KWAKE
Hifadhi ya Taifa ya Katavi ilianzishwa mnamo mwaka 1974. Inapatikana kwa  njia ya  usafiri wa barabara  takribani  kilomita  40  Kusini  Mashariki mwa  mji wa Mpanda. 

ENEO LAKE:
Ukubwa wa eneo la hifadhi hii ya Katavi ni Kilomita za mraba 4,471.

UFIKAJI HIFADHINI:
Hifadhi ya Taifa  ya Katavi  inafikika  kwa njia  ya usafiri wa barabara  kiasi cha umbali  wa Kilomita  40  kutoka  katika  Mji wa Mpanda. Ni sawa na saa 1 katika uendeshaji wa gari wa mwendo wa kawaida. Vile  vile  hifadhi  hii  inaweza  kufikika  kwa  kutumia  njia ya barabara ya  Kigoma  na Mbeya  inayopitia  Katavi.

soma zaidi

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
walio tembelea

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU