UJUMBE KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI

Ukweli wa mambo ulio wazi na usiofichika  si Watanzania Wazalendo wote  nchini  Tanzania wanaofahamu  kwa undani na umakini mkubwa  na hata vile vile  kupata  fursa  ya kuvitembelea  vivutio vyetu asilia  vya  utalii  vilivyo  tajiri na ulio urithi  wetu tuliopewa na  mwenyezi Mungu  kama  vile  maeneo  ya kihistoria  na tamaduni pamoja  na maeneo  yetu mbalimbali   ya  uhifadhi  ya   mbuga za wanyamapori  na kadhalika. Fursa  zaidi  ambayo  wananchi  wetu  wanayopata  ni  katika  maonyesho  ya  biashara  ya kimataifa  kama vile  sabasaba au nane nane na  haishangazi  kuona  ya kwamba  Mtanzania  mzalendo  anakuwa  mgeni  ndani ya  nchi  na  kushangaa shangaa kuliko  mgeni  kutoka nje  ya nchi. 

          Ukweli wa mambo  uliowazi na usiofichika  ni ya  kwamba  takwimu  zinaonyesha  kuwa taasisi  za kielimu  kama vile  vyuo  mbalimbali, shule za sekondari  na msingi  pamoja na sekta  binafsi  na za umma  ndio zinazochangia  kuongezeka  kufanya  idadi  ya watanzania  watalii wa ndani  kuwa kubwa  ingawa  bado  kabisa haitoshelezi. 

          Tarehe  9/12/2011, nchi yetu  Tanzania na Watanzania  tulisheherekea  na kuadhimisha  miaka 50 ya uhuru wa taifa  letu. Miaka 50 ya Uhuru  wa Taifa letu  yenye  wakazi zaidi  ya watu  milioni 40,000 na bado haishangazi   kuona  ya kwamba  idadi  ya watanzania  wazalendo  watalii wa ndani  haizidi  milioni  mbili. Vile  vile  idadi  ya watalii  kutoka nje  ya nchi  ni  kubwa zaidi  kuliko  watanzania  watalii wa  ndani.  Hii  inamaanisha  ya  kwamba   nguvu  kubwa  kupindukia  imewekezwa  kwa wageni  watalii  kutoka  nje ya nchi. Kwa mfano hai,  takwimu za utalii za mwaka 2009  zilionyesha  idadi ya watanzania wazalendo  watalii  wa ndani  ilikuwa  660,000. Mwaka  uliofuata  2010  idadi hiyo  ya  watanzania  watalii  wa ndani  ilishuka  na kufikia  550,000.

          Kwa sababu  hii ndio  iliyotupelekea  sisi  kama  sehemu  ya watanzania  wengineo  nchini Tanzania kama  taasisi  ya kielimu  katika  sekta  ya  utalii  kuisaidia serikali  yetu  na  wizara  yake  mama ya mali asili  na utalii  kuanzisha  tovuti  hii ya  kuwaelimisha  na kuwahamasisha  watanzania  wazalendo  popote  pale  walipo  ya  kwamba wanaweza  na si wageni  tu kutoka  nje ya  ya nchi. 

          Hivyo  basi  ni wakati  muafaka  wa bodi ya utalii nchini Tanzania na wadau  wengineo  mbalimbali  katika  sekta ya  utalii na  hali  kadhalika   taasisi za kielimu  kufanya  kazi kwa  ukaribu  na wizara  ya mali  asili  na utalii  katika  kushiriki  zaidi kizalendo  katika  kueleimisha  na kuhamasisha  watanzania  kuwa na utamaduni  wa  kutembelea  vivutio vya utalii  nchini  ulio  urithi wetu. Inawezekana  kabisa  kwa mimi na wewe  kama watanzania  wenye  uzalendo  wa nchi  na watu  wake  wote tukitimiza  wajibu  wetu  kwa  vitendo.

 

 

“Usiulize Tanzania na watanzania watakufanyia nini?
Jiulize  utaifanyia nini Tanzania na Watanzania”
Edgardo  Kabulwa Welelo 20/10/2011

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
walio tembelea

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU